Lifestyles

Tips Kwa Zawadi za Kiume

Sunday, February 12, 2017 Naomi Mwakanyamale 0 Comments
Unapotoa zawadi  kwa mtu yeyote kwanza jua aina ya mahusiano mliyonayo na huyo mtu, ndipo utafute aina ya zawadi inayoendana na mahusiano yenu. SIYO KILA ZAWADI NI YA KILA MTU.


GIFTS IDEAS FOR MEN
Saa ya mkononi:-
Aina hii ya zawadi waweza mpa mtu yeyote yule. Haijalishi. Hapo inategemea na uwezo wako. Zipo saa za  Elfu mpaka mamilion. Nguvu yako.


Begi la Laptop:-

Hii pia waweza mnunulia mtu yeyote na wakati wowote.Key holder:-
Kila mtu anazofungua. Kwa hiyo ni moja ya zawadi ambayo kila mtu angehitaji

House Tools:-
Kwa mwanaume yeyote awe anaishi kwake, ameoa, hajaoa, angehitaji vifaa vya kurekebisha mambo madogo madogo yanayoharibika kwenye nyumba anayoishi kabla hajakimbilia kuita fundi.


Wallet:-

Hii ni zawadi kwa yeyote na inategemea na pesa uliyonayo.Shati:-
Hapo pia inategemea na kiwango cha pesa na waweza mpa mtu yeyote yule. Haijalishi aina ya mahusiano. Yapo mashati ya kila bei.

Suti:-
Unaweza mnunulia yeyote yule, na inategemea na uwezo wako. Lakini hata mke kama upo karibu na mavazi ya mumeo, ukajua size zake, siyo zawadi mbaya kununua
kwenye kumbukumbu fulani fulani za mwaka, hasa unapotaka kutoka naye wewe, au kwenye tukio lake la kihistoria kama siku yake ya kupandishwa cheo. Utaweka kumbukumbu kwenye maisha yake. Kila akikumbuka lile tukio, na wewe atakumbuka ulihusika kufanikisha.Perfume:-
Sio wanaume wote wanaopendelea kupaka perfume. Aidha kwa mazoea, uwezo, kutofikiria, naamaanisha kutoona umuhimu wake au wengine wana allergies. Inategemea na uwezo wako.
Unaweza kuanza na body spay. Pia ikamfanya mpenzi wako akanukia vizuri. Ukipata yenye harufu nzuri, unaweza usione tofauti na perfume, japo perfume inadumu kwa muda mrefu kwenye nguo.


Nguo za Ndani:-
Hapa ni kwa wanandoa.
Ungalifu katika hili ni muhimu na inategemea na mazingira. Lakini sio mbaya ukahusika na ubadilishaji wa nguo za ndani za mumeo, mara kwa mara. Sio lazima ikawa ni siku kuu tu.
Hapa wife anajukumu la kuangalia nguo za ndani za mumewe na kujua aina ya nguo za ndani anazopendelea. Sio wote wanao vaa briefs. JUA NI KITU GANI MPENZI WAKO ANAPENDELEA.
Hapo ikiwemo Socks. Usiache mumeo anatembea na socks zilizotoboka. Au usinunue aina ya socks zinazofanya miguu yake ikanuka. Na kama anatatizo la kunuka mguu, tafuta dawa. ZIPO dawa za kutibu tatizo hilo.

Sabuni ya kuogea na Lotion:-
Mzoee mumeo kwa harufu fulani. Mnunulie aina fulani ya sabuni ya kuogea ambayo unajua itakata harufu ya jasho na kumfanya mumeo anukie vizuri siku nzima. Hapa ni kwa manufaa yako na yeye. Mwanaume anayenukia vizuri, ni rahisi hata kupata kiss muda na wakati wowote. Mnunulie na Lotion itakayomfanya mumeo asipauke au
itakatomfanya awe na siku ambayo hata yeye mwenyewe anajihisi fresh. Usisahau nyayo zake pale upatapo nafasi. Mwanamke kumbuka miguu ya mumeo. Mpake wewe mwenyewe lotion hiyo kila upatapo nafasi. Kwenye nyayo safi na katikati ya vidole ulivyovikata kucha, ukasafisha na kukausha na taulo. Hasa nyakati za usiku kabla hajakwenda kulala.

Deodorant:-
Hii ni zawadi kwa yeyote.  Usiache mwenzako akanuka mpaka shati linaweka harufu ya jasho. Mtafutie deodorant ya bei yeyote, mpe. Hata ukiwa na rafiki, AU mfanyakazi mwenzako anayenuka, bosi, yeyote yule. Tafadhali tafuta sikukuu yake anayosherekea, mpe deodorant kama zawadi, endapo utashindwa kumwambia moja kwa moja. Wapo wenye sensitive skin. Akipaka aina fulani ya deodorant anawashwa. Kama ni mtu uliyenaye karibu, hakikisha kila unapomnunulia wakati mwingine, nunua DEODORANT FOR SENSITIVE SKIN.

CHENI:-
Wapo wanaume wanaopendelea kuvaa cheni za shingoni au mkononi. Unaweza nunua ikawa moja ya zawadi. Tafuta accesories za wanaume, angalia kama kuna itakayomfaa.

Viatu:-


Sio lazima vikawa viatu vya kutokea. Yaani Special occasion. Mtafutie viatu atakavyoweza kuzunguka navyo mara kwa mara. kwenye shuguli zake za kawaida.


Na kama ni mtu wa
mazoezi, au unataka aanze mazoezi, sio vibaya kumpa viatu na nguo za mazoezi kama motivation.

Mtoe:-
Tumeshazoe sisi wanawake kutolewa na waume zetu mara zote. Lakini hata wewe unaweza kumtoa mumeo. Tafuta pesa yako ya pembeni, mtoke wewe na yeye tu. Ili kupata muda wa peke yenu.
Lakini kama uwezo hakuna, hiyo siyo sababu yakuwafanya msipate faragha. Tokeni mkiwa mmevaa kawaida tu, tafuteni sehemu ambayo mtapata nafasi yakuongea nyinyi wenyewe, mbali na nyumbani na mbali na watoto. Ni muhimu sana kwa wanandoa kupata huo wakati.

HIZO NI BAADHI TU YA ZAWADI KWA AJILI YAKE. NAJUA ZIPO NYINGI SANAAA. NARUDIA, INATEGEMEA NA MTU UNAYETAKA KUMPA ZAWADI HIYO. KUWA MAKINI USICHANGANYE ZAWADI ZA MPENZI NA RAFIKI WA KAWAIDA AU WATU UNAOWAHESHIMU. UNAWEZA KUHARIBU. 
                     *KILA LA KHERI*


0 comments: